QUITO. Amri yatolewa kumkamata rais wa zamani wa Ecuador.
21 Aprili 2005Matangazo
Rais mpya wa Ecuador, Afredo Palacio, ameamuru kukamatwa kwa kiongozi wa zamani, Lucio Gutierrez, aliyefutwa kazi na bunge hapo jana. Kutimuliwa kwake kulifuatia juma moja la maandamano katika mji mkuu Quito, ambapo waandamanaji walimtaka kanali huyo wa zamani katika jeshi la taifa, ajiuzulu kwa kuingilia shughuli za mahakama kuu nchini humo.
Wabunge 60 walipiga kura kumuondoa madarakani Gutierrez kwa kile walichokiita hatua ya kiongozi huyo kuwacha jukumu lake na kuingilia kazi nyengine. Upinzani kwa upande wake umemlaumu kiongozi huyo kwa ufisadi. Brazil imetangaza Gutierrez amejificha katika ubalozi wake mjini Quito.