PYONGYANG:Wakuu wa Korea Kusini na Kaskazini katika mkutano wa kihistoria
8 Agosti 2007Viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini wanatarajiwa kuwa na mkutano wao wa pili katika historia ya nchi hizo mbili.
Rais Roh Moo-Hyun atakutana na mwenzie Kim Jong-il wa Korea Kaskazini katika mji mkuu wa Korea Kusini Pyongyang mwisho wa mwezi huu.
Mkutano huo utafanyika ikiwa ni miaka saba toka ule wa kwanza kati ya kiongozi wa Korea Kusini Kim alipokutana na kiongozi wa wakati huo wa Korea Kusini Kim Dae-jung.
Kwa upande mwengine, Korea Kaskazini imeendelea kuwa na mazungumzo na mataifa mengine matano kuangalia jinsi ya kufikia suluhu la vinu vyake vyake vya nuklia.
Nchi hizo tani, Marekani, Uurusi, China, Japan na Korea Kusini zimezungumzia misaada zaidi kwa Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo kufunga vinu vyake vya nuklia vilivyoko Yongbyon mwezi uliyopita .
Iwapo Korea Kaskazini itafunga vinu vyake vyote itapata msaada wa tani 950,000 za nishati ya mafuta ikiwa ni pamoja na faida kubwa katika nyanja za kidiplomasia na kiusalama.