1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG:Viongozi wa Korea Kusini na Kaskazini wakutana Pyong Yang

17 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF2l

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong il amefanya mkutano wa aina yake na kiongozi wa ngazi ya juu wa Korea kusini mjini Pyong Yang.

Mkutano huo wa viongozi hao wawili umefanyika wakati ambapo kuna wasiwasi wa iwapo Korea kaskazini itarejea kwenye meza ya mazungumzo ya pande sita juu ya mpango wake wa nuklea.

Wajumbe wa Korea kusini walikuwa wamekutana Pyong yang kuadhimisha miaka mitano ya kufanyika mkutano muhimu kati ya kiongozi huyo na rais wa korea kusini Kim Dae-Jung.

Duru ya mwisho ya mazungumzo juu ya mpango wa Nukelea wa Korea kaskazini ulifanyika mwezi Juni mwaka jana.