PYONGYANG:Korea Kaskazini imefunga kinu chake cha nyuklia
16 Julai 2007Matangazo
Wakaguzi wa umoja wa mataifa wamethibithisha kuwa Korea Kaskazini imekifunga kinu chake cha nyuklia cha Yongbyon.
Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia Mohamed El Baradei amesema kuwa Korea Kaskazini inatoa ushirikiano na kwamba hatua itakayofuatwa na wakaguzi hao wa umoja wa mataifa ni kuhakikisha kuwa vituo vingine vya Korea Kaskazini pia vinasimaisha shughuli zake.
Mjumbe wa Marekani Christopher Hill amesema kuwa hatua ya kukifunga kinu cha Yongbyon ni hatua ya kwanza ya kuvibomoa vituo vyote vya nyuklia nchini Korea Kaskazini.
Mkutano wa pande sita utakao jadili kumaliza kabisa shughuli za kinyuklia za Korea Kaskazini utafanyika mjini Beijing China siku ya jumatamno.