1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Urusi na Korea Kusini yaulaani mpango wa Korea Kaskazini wa jaribo la kinyuklia

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD63

Urusi na Korea Kusini zimeulaani vikali mpango wa Korea Kaskazini wa kutaka kufanya jaribio la kinyuklia zikisema mpango huo hauwezi kukubalika.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Urusi na Korea Kusini wamesema hatua ya serikali ya mjini Pyongyang itazidisha ugomvi na kuyafanya mazungumzo ya mataifa sita yachelewe na kuwa vigumu kuanza.

Tangazo la Korea Kaskazini juzi Jumanne kwamba inapanga kufanya jaribio la kinyuklia limezusha hali ya wasiwasi na kukosolewa na jumuiya ya kimataifa. Serikali ya Pyongyang haikutaja tarehe ya jaribio hilo, lakini ilisema inataka kufanya hivyo kufuatia kuongezeka kwa uhasama wa Marekani dhidi yake.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likifanya mashauriano vipi kujibu tangazo hilo la Korea Kaskazini.

Wakati haya yakiarifiwa, kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong II hajaonekana hadharani kwa siku 20. Inadhaniwa hataki kuonekana kabla jaribio la kinyuklia kufanywa.