PYONGYANG: Majadiliano ya mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini
14 Machi 2007Matangazo
Korea ya Kusini inasem,haikuona ishara yo yote kuwa Korea ya Kaskazini inafunga kituo chake kikuu cha nyuklia,ambalo ni sharti kuu la makubaliano muhimu yaliyopatikana mwezi uliopita. Makubaliano hayo yametoa wito wa Korea ya Kaskazini kukifunga kinu hicho katika kipindi cha siku 60 na badala yake nchi hiyo kupewa msaada wa nishati.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia,Mohamed el-Baradei hivi sasa yupo Pyongyang kwa majadiliano ya kutekeleza masharti yaliyokubaliwa.