PYONGYANG: Korea ya Kaskazini yafunga kinu cha nyuklia
15 Julai 2007Matangazo
Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wanajiandaa kuhakikisha tangazo la Korea ya Kaskazini kuwa imeufunga mtambo wake wa nyuklia wa Yongbyon. Mjumbe mkuu wa Marekani,Christopher Hill akikaribisha hatua hiyo kwa hadhari amesema huo ni mwanzo wa kupunguza silaha.Wakati huo huo msemaji wa wizara ya nje ya Marekani,Sean McCormack amesema,Washington inangojea hatua itakayofuata ambapo Korea ya Kaskazini inatazamiwa kuitangaza miradi yake yote ya nyuklia na kusitisha ile iliyopo hivi sasa.Siku ya Jumamosi,Korea ya Kaskazini ilipokea tani 6,200 za mafuta.Hatua zingine zinatazamiwa kukamilishwa siku ya Jumatano mjini Beijing wakati wa majadiliano ya pande sita,zikiwepo Korea zote mbili,Marekani,China,Japani na Urusi.