1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Korea ya Kaskazini itayari kuachilia mbali miradi ya nyuklia

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhL

Korea ya Kaskazini ipo tayari kufunga mitambo yake yote ya nyuklia mwaka huu.Hiyo ni kwa mujibu wa wajumbe wa kimataifa wanaoshiriki katika majadiliano yanayohusika na kusitishwa mradi wa nyuklia wa Pyongyang.Tangazo hilo limetolewa saa chache baada ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuthibitisha kuwa mitambo mitano mikuu ya nyuklia ya Korea ya Kaskazini imeshafungwa.Maendeleo hayo yamezidisha matumaini kuwa makubaliano yalioisadikisha Korea ya Kaskazini kuachilia mbali miradi yake ya silaha za nyuklia na badala yake kupewa misaada,sasa yameanza kuzaa matunda kufuatia majadiliano ya miaka na miaka.