PYONGYANG: Korea Kaskazini yaonya itafanya majaribio mengine ya nyuklia
11 Oktoba 2006Matangazo
Korea Kaskazini imeonya leo kwamba vikwazo vyovyote vikali dhidi yake kufuatia jaribio lake la kinyuklia, vitaonekana kama kutangaza vita dhidi yake.
Naibu kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yong Nam, amesema uamuzi wa kufanya majaribio zaidi utategemea hatua zitakazochukuliwa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini.
Aidha kiongozi huyo amesema sera za Marekani kuelekea Korea Kaskazini ndizo zitakazoamua ikiwa nchi hiyo itarudi kwenye mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wake wa kinyuklia yaliyokwama.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amtoa mwito hatua kali zichukuliwe dhidi ya utawala wa Korea Kaskazini.