1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Korea Kaskazini kufunga kinu chake cha nyuklia

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSb

Korea kaskazini itakifunga kinu chake cha nyuklia cha Yongbyon, shina la mpango wake wa nyuklia, na pia kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kwenda katika kinu hicho kama sehemu ya kupokonywa silaha ya makubaliano yaliyofikiwa mjini Beijing, China hii leo.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Korea Kaskazini inatakiwa kuchukua hatua hizo katika siku 60. Itakapofanya hivyo itapewa tani elfu 50 za mafuta au msaada wa kiuchumi ulio na thamani ya kiwango hicho cha mafuta. Mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yalianza Alhamisi wiki iliyopita mjini Beijing.

Makubaliano yaliyofikiwa leo yameumaliza mkwamo wa miaka mitatu wa mazungumzo hayo. Hapo awali mjumbe wa Marekani katika mazungumzo hayo, naibu waziri wa mambo ya nje, Christopher Hill, alitangaza baada ya mazungumzo yaliyodumu muda wa saa 16 kwamba makubaliano ya kwanza yamefikiwa. Marekani haijayapa uzito makubaliano hayo.