1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Hatua ya kwanza ya kufunga mtambo wa nyuklia

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiI

Korea ya Kaskazini imetangaza kuwa imefunga mtambo wake wa nyuklia wa Yongbyon.Wakaguzi wa nishati ya atomu wa Umoja wa Mataifa,wapo nchini Korea ya Kaskazini kusimamia hatua ya kufunga mtambo huo.

Mjumbe wa Marekani,Christopher Hill amesema, kufungwa kwa mtambo huo ni hatua ya kwanza. Akaongezea kuwa hatua hiyo itakuwa na maana tu kama hatua zaidi zitachukuliwa - na zipo kazi nyingi za kufanywa.

Wakati huo huo,mwanadiplomasia wa Korea ya Kaskazini amesema,serikali ipo tayari pia kuweka wazi miradi yake ya nyuklia kama haitowekewa vikwazo na Marekani.