1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONG YANG:Azimio juu ya Korea Kaskazini lapitishwa na IAEA

1 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVs

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nguvu za nishati ya Atomiki IAEA limepitisha azimio la kukubali mapatano yaliyofikiwa na Korea kaskazini ya kuachana na mpango wa silaha za Nuklia.

Azimio hilo limefuatia mazungumzo ya pande sita yaliyofanyika kuanzia septemba 19 mjini Beijing hii ikiwa ni hatua ya kwanza kuelekea lengo la kuachana na mpango wa Nuklia wa Korea Kaskazini kwa njia ya amani.

Wakati huo huo mjumbe wa Marekani Chrispher Hiil amepinga sharti la Korea kaskazini la kutaka kupewa muda wa kuiruhusu kusimamisha shughuli zake za kinuklia kuelekea hatua ya kumaliza kabisa shughuli za kutengeneza silaha za Nuklia.