1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin, Xi kuzungumza kesho Ijumaa- Kremlin

29 Desemba 2022

Rais wa Urusi Vladmir Putin atafanya mazungumzo kwa njia ya video na kiongozi wa China Xi Jinping kesho Ijumaa, wakati Urusi ikitafuta kuimarisha mahusiano na Beijing.

https://p.dw.com/p/4LXUV
Russland I Vladimir  Putin
Picha: Sergei Karpukhin/AP/picture alliance

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amewaambia waaandishi habari leo kuwa utakuwa mkutano muhimu wa kubadilishana mawazo kuhusu matatizo makubwa ya kikanda, ambayo yote yanayahusu madola hayo mawili. Putin anataka kuimarisha mahusiano na Beijing na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika wakati ambapo analaaniwa na jamii ya kimataifa na kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine. Urusi na China mwezi huu zilifanya mazoezi ya pamoja ya jeshi la majini, ambayo mkuu wa jeshi la Urusi alielezea kuwa ni jibu la uchokozi wa jeshi la Marekani katika kanda ya Asia Pasifik. Wiki iliyopita, Urusi alizindua kisima cha gesi mashariki mwa Siberia ambacho kitairuhusu Urusi kuongeza uuzaji wa bidhaa hiyo nchini China huku nchi za Magharibi zikikusudia kusitisha utegemezi wao kwa Moscow.