1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Watu wa itikadi kali walihusika na shambulizi Moscow

26 Machi 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin amekiri kwa mara ya kwanza kuwa watu itikadi kali ndio waliohusika na shambulizi la wiki iliyopita kwenye ukumbi wa tamasha la muziki nje ya mji mkuu Moscow.

https://p.dw.com/p/4e76U
Rais wa Urusi Valdimir Putin
Rais Putin amesema kuwa wahusika wa shambulio la Moscow walikuwa wa itikadi kali za kiislamuPicha: Kremlin.ru/REUTERS

Putin amesema katika mkutano uliorushwa kwenye televisheni kuwa wanafahamu uhalifu huo ulifanywa na watu wa misimamo mikali, ambao itikadi yao imekuwa ikipingwa na ulimwengu wa Kiislamu kwa karne nyingi.

Soma pia: Macron asema IS imehusika katika shambulizi la Moscow

Lakini kiongozi huyo wa Urusi alisema maswali mengi bado hayajajibiwa, ikiwa ni pamoja na ni kwa nini washambuliaji hao walijaribu kukimbilia Ukraine -- madai ambao Kyiv imeyapinga. Amesema uhalifu huo huenda ukawa kiunganishi katika mfululizo mzima wa majaribio ya wale ambao wamekuwa katika vita na Urusi tangu mwaka wa 2014.

Aliyasema hayo bila kuitaja Ukraine na washirika wake. Watu 11 walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo lililotokea katika jengo la Crocus City Hall. Watu wenye silaha walivamia na kuanza kuwafyatulia risasi washiriki wa tamasha la muziki kabla ya kulichoma moto jengo hilo na kuwauwa karibu watu 139. Watu wengine 180 walijeruhiwa.