1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Putin awasili Korea Kaskazini katika ziara ya nadra

19 Juni 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili Korea Kaskazini katika ziara ya nadra inayoashiria kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4hDxf
Putin akisalimiana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipowasili Pyongyang.
Putin akisalimiana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipowasili Pyongyang. Picha: Yonhap/picture alliance

Putin amepokewa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika uwanja wa ndege wa Pyongyang, na wawili hao wamekumbatiana kabla ya kuelekea katika nyumba ya wageni ya Kumsusan ambako Putin atakaa.

Soma pia: Putin kusaini mikataba ya ushirikiano wakati wa ziara mjini Pyongyang

Putin anayefanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika muda wa miaka 24, ameeleza katika taarifa iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari vya serikali saa chache kabla ya kuwasili kwake, kuwa anashukuru uungwaji mkono wa Korea Kaskazini kwa oparesheni maalum ya kijeshi ya Urusi ndani ya ardhi ya Ukraine.

Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini limeelezea mkutano kati ya Putin na Kim Jong Un kama tukio la kihistoria linaloonyesha uimara wa urafiki wa dhati na umoja kati ya mataifa hayo mawili.