1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin afanya ziara nchini Vietnam

Josephat Charo
20 Juni 2024

Ziara ya Putin Vietnam itachochea ushirikiano wao wa kimkakati na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kupitia biashara na uwezekani.

https://p.dw.com/p/4hHNK
Rais Vladimir Putin wa Urusi akiwasili mjini Hanoi 20.06.2024
Rais Vladimir Putin wa Urusi akiwasili mjini Hanoi 20.06.2024Picha: Minh Hoang/AP Photo/picture alliance

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili mjini Hanoi nchini Vietnam kwa ziara ya kiserikali kufuatia mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Hayo yameripotiwa na afisi ya rais wa Urusi.

Putin anafanya ziara katika mji mkuu wa Vietman kufuatia mualiko wa Mkuu wa chama cha Kikomunisti Nguyen Phu Trong. Rais Putin amewasili Hanoi akitokea Korea Kaskazini alikoondoka jana jioni baada ya kufanya ziara ya siku mbili.

Hivi leo Putin atashiriki hafla ya kukaribishwa katika ikulu ya rais kabla kuhudhuria mazungumzo ya pande mbili na mkuu wa chama cha kikomunisti Trong.

Soma pia: Rais Putin anazuru mji wa Hanoi

Putin pia atakutana na waziri mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh na raia wa Vietnam waliosomea nchini Urusi. Putin pia atahudhuria dhifa ya kitaifa.