1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin aapa majaribio zaidi ya kombora lililorushwa Ukraine

23 Novemba 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameahidi kufanya majaribio zaidi ya kombora jipya la masafa ya kati lililorushwa Ukraine. Hayo ni wakati Rais wa Ukraine akitoa witowa kupewa mifumo mipya ya ulinzi wa angani.

https://p.dw.com/p/4nLK6
Zima moto wakiudhibiti moto uliotokana na kombora la Urusi kwenye mji wa Dnipro, Ukraine
Rais wa Urusi Putin amesema kutakuwa na majaribio zaidi ya kombora jipya la OreshnikPicha: Press Service of the State Emergency Service of Ukraine in Dnipr/picture alliance

Kauli za karibuni kutoka kwa viongozi hao zilijiri saa chache tu baada ya bunge la Ukraine kusitisha shughuli zake kuhusiana na ongezeko la hofu ya shambulizi la kombora.

Soma pia:

Siku moja baada ya Moscow kufyatua kombora jipya kwenye mji wa Ukraine wa Dnipro, Putin amesema kutakuwa na majaribio zaidi ya kombora jipya la Oreshnik. Akizungumza kwenye mkutano na viongozi wa kijeshi wa Urusi, Putin amesema Urusi pia itaanza kutengeneza makombora hayo kwa wingi.

Rais Zelensky wa Ukraine amesema tayari anatafuta mifumo mipya ya ulinzi wa angani kutoka kwa washirika wake. Putin alidokeza kuwa mashambulizi yanayofanywa na Ukraine ndani ya maeneo ya Urusi kwa kutumia makombora inayopewa na washirika wa Magharibi yanaongeza hofu ya vita hivyo kuenea na kuwa mgogoro wa kidunia.