1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PSG wafungua mwanya wa pointi 8 dhidi ya Nice

15 Januari 2024

Klabu ya Nice iliyoanza vyema msimu wa ligi ya Ufaransa Ligue 1 kwa mechi 13 bila kufungwa na kuwa katika nafasi ya kuwania ubingwa, imepata kipigo chake cha tatu msimu huu,tangu kulazwa kwa mara ya kwanza na Nantes.

https://p.dw.com/p/4bGRT
UEFA Champions League PSG - Milan
Kylian Mbappe akisherehekea na wachezaji wenzake wa PSGPicha: FRANCK FIFE/AFP

Katika mechi tano za ligi zilizopita wameshindwa tatu mechi zote walizoshindwa ikiwa ni ugenini ila licha ya hilo bado wangali kuishikilia nafasi ya pili.

La kutia wasiwasi lakini ni mwanya unaozidi kuongezeka kati yao na vinara Paris Saint Germain unaotia wasiwasi.

PSG walipata ushindi wa 2-0 mwishoni mwa wiki dhidi ya Lens na sasa tofauti iliyoko kati yao na Nice ni pointi nane.

Chanzo: Reuters/AP/AFP