Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, anasema hatua ya Rais John Pombe Magufuli kumchukuwa tena Prof. Sospeter Muhongo kwenye wizara ya nishati na madini ambayo alilazimika kujiuzulu kwenye awamu iliyopita ni kosa la kisiasa linalotia shaka vita dhidi ya ufisadi.