1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA: Kikosi cha NATO chatumwa Kosovo

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIa

Shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO, limeanza kupeleka wanajeshi zaidi kwenda katika jimbo la Kosovo. Hiyo ni sehemu ya juhudi za kawaida za kulinda amani katika mkoa huo wa Serbia unaotawaliwa na Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa NATO wamesema wanajeshi 600 wa Ujerumani watashiriki katika mazoezi ya kijeshi kupata uzoefu wa mazingira ya Kosovo.

Kupelekwa kwa wanajeshi hao kunafanyika wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kujadili mpango uliozusha utata wa kulipa uhuru jimbo la Kosovo kutoka kwa Serbia.

Walbania wa Kosovo walio wengi wameliunga mkono pendekezo hilo ingawa limepingwa vikali na serikali ya Belgrade.