Prinz na Zidane mabingwa wa kimataifa wa kabumbu:
15 Desemba 2003Matangazo
BASEL: Mchezaji mwanamke wa kambumbu wa taifa wa Ujerumani Birgit Prinz na Mfaransa Zinedine Zidane wamechaguliwa wachezaji bora kabisa wa kabumbu wa mwaka huu, kwa kulingana na matokeo ya uchaguzi wa makocha wa taifa wa Shirika la Kimataifa la Kabumbu. Zidane anachaguliwa kwa mara ya tatu akiwapiku Thierry Henry wa Ufaransa na Ronaldo wa Brazil.