1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA: Zimbabwe huenda ikasaidiwa sehemu ya madeni yake

25 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEr5

Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini amesema nchi yake huenda ikachukua sehemu ya madeni ya kigeni ya Zimbabwe.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Pretoria,Mbeki alisema kuwa mazungumzo yanaendelea pamoja na aserikali ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.Amesema Afrika ya Kusini inataka kuzuia mporomoko wa uchumi nchini Zimbabwe na huenda ikachukua sehemu ya deni la Zimbabwe la Dola bilioni 4 na nusu.Zimbabwe inakabiliwa na mzozo mkubwa kabisa wa kiuchumi tangu kujipatia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1980.Wiki iliyopita vyombo vya habari nchini Zimbabwe viliripoti kuwa serikali ya Mugabe iliomba mkopo wa Dola bilioni moja kununua chakula na mafuta ya petroli na pia kujiepusha kufukuzwa kutoka Fuko la Fedha la Kimataifa IMF kwa sababu ya kuchelewa kutoa malipo ya Dola milioni 300.