1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA: Wachimba-migodi wagoma kazi

9 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmj

Kiasi ya wafanyakazi 100,000 katika migodi ya dhahabu nchini Afrika ya Kusini wamegoma kazi kwa mara ya kwanza tangu miaka 18,wakidai kuongezewa mishahara.Mgomo huo umefanywa baada ya kutofanikiwa kwa majadiliano kati ya makampuni 4 na Muungano wa Taifa wa wachimba-migodi.Nchini Afrika ya Kusini migodi ya dhahabu huchangia asilimia 8 ya pato la ndani.Hata baada ya kuondoshwa kwa utawala wa ubaguzi wa kikabila,nchini humo bado kuna pengo kubwa la mapato.Kwa sababu ya hali ya kutoridhika,hivi karibuni,wafanyakazi kwenye idara za miji, madukani na shirika la ndege la taifa waligoma kazi.