1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

Prabowo wa Indonesia ajitapa kuwa atashinda urais wiki ijayo

11 Februari 2024

Mgombea anayeongoza uchunguzi wa maoni ya umma katika kinyang´anyiro cha kuwania urais nchini Indonesia Prabowo Subianto amesema ana matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo

https://p.dw.com/p/4cGw4
Kamanda wa zamani wa jeshi la Indonesia  Prabowo Subianto akishiriki mdahalo wa urais ulioandaliwa Februari 4, 2024
Kamanda wa zamani wa jeshi la Indonesia Prabowo SubiantoPicha: KPU

Prabowo, kamanda wa zamani wa jeshi, ni miongoni mwa wagombea watatu wanaochuana kuchaguliwa kuwa rais wa Indonesia katika uchaguzi huo wa Februari 14.

Prabowo anaamini ataibuka mshindi kupitia duru moja ya uchaguzi

Amesema anaamini atatangazwa mshindi kupitia duru moja tu ya uchaguzi na kuwa rais wa taifa hilo la tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa yale yanayotawaliwa kidemokrasia.

Mgombea anapaswa kupata asilimia 50 ya jumla ya kura zote za ngazi ya taifa na asilimia 20 kwenye nusu ya majimbo ya nchi hiyo ili kutangazwa mshindi.

Wapinzani wa Prabowo

Hadi sasa uchunguzi wa maoni ya umma unaonesha Prabowo amevuka kiwango hicho cha asilimia 50. Wapinzani wake wakuu ni gavana wa zamani wa mji mkuu wa Jakarta,  Anies Baswedan na aliyekuwa gavana wa jimbo la Java Ganjar Pranowo.