1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM: Mkutano wajadili mabadiliko ya hali ya hewa

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIG

Mawaziri wa mazingira wa nchi nane tajiri zilizoendelea kiviwanda-G8 na wa madola makuu matano yanayoendelea,wanakutana katika mji wa Potsdam,mashariki mwa Ujerumani kujadili njia za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Waziri wa mazingira wa Ujerumani,Sigmar Gabriel ambae ni mwenyeji wa mkutano huo amesema,nchi za G8 na mataifa yanayoendelea zinapaswa kushirikiana kupiga vita ongezeko la joto duniani.Hata hivyo lakini hakuna matarajio kuwa makubaliano timamu yatapatikana katika mkutano huo.Marekani imeshasema waziwazi,kwa hivi sasa haitaki kujihusisha na malengo ya kujifungamanisha.Mkutano wa Potsdam unafanywa huku shirika moja la Kimarekani likiripoti kuwa kati ya Desemba na Februari kipimo cha ujoto wa ardhi kilifikia kiwango cha juu kabisa tangu kuanzishwa utaratibu wa kupima hali ya hewa,zaidi ya karne moja iliyopita.