POTSDAM: mawaziri wamaliza mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa
18 Machi 2007Matangazo
Mawaziri wa nchi tajiri nane duniani,wamemaliza mkutano wao na mawaziri wanzao kutoka nchi zinazoinukia kiuchumi uliofanyika katika mji wa Potsdam Ujerumani juu ya hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Waziri wa mazingira wa Ujerumani bwana Sigmar Gabriel ametoa mwito juu ya kuwapo mwambatano baina ya kukabiliana na mabadiliko ya hewa na maendeleo ya uchumi.