1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORTOROZ: Sergei azikosoa nchi za NATO

29 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7e

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Ivanov, amezilaumu nchi wanachama wa shirika la NATO kwa kuiuzia Georgia silaha zinazotengezwa kutoka Soviet.

Waziri Ivanov alikuwa akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na mawaziri wa shirika la NATO mjini Potoroz nchini Slovenia. Hata hivyo amekataa kuyataja mataifa husika, lakini akasema ni miongoni mwa wanachama wapya wa NATO, akiashiria mataifa 10 yaliyojiunga na shirika hilo mnamo mwaka wa 2004.

Sergei Ivanov ametoa matamshi hayo wakati hali ya wasiwasi ikizidi kati ya Georgia na Urusi. Kiongozi wa shirika la NATO, Japp de Hoop Scheffer, amezitolea mwito Georgia na Urusi kumaliza mgogoro huo wa wanajeshi waliokamatwa.

´Mwito huu ni kwa Georgia na marafiki zetu wa Urusi. Lakini hilo si jambo ambalo NATO itajishuhulisha nalo moja kwa moja.´

Mapema leo Urusi iliwaondoa baadhi ya wanadiplomasia wake ikitaka maofisa wake wa jeshi wanaozuiliwa kwa kushukiwa kuwa makachero waachiliwe huru.