1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORTOROZ: NATO kuongoza vikosi vyote vya usalama

28 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7z

Mawaziri wa ulinzi wa shirika la kujihami NATO wamekubaliana kuchukua uongozi kamili wa vikosi vya amani kote Afghanistan.Uamuzi huo unamaanisha kuwa wanajeshi 10,000 wa Marekani walio mashariki mwa Afghanistan watakuwa chini ya uongozi wa NATO katika muda wa majuma machache yajayo.NATO tayari huongoza wanajeshi 20,000 kutoka nchi 37 mbali mbali.Vikosi hivyo vipo sehemu za kaskazini, magharibi na kusini mwa Afghanistan pamoja na mji mkuu Kabul.Kutoka jumla hiyo,wanajeshi 3,000 wa Ujerumani wapo kaskazini mwa Afghanistan na mamlaka ya ujumbe huo yanamalizika tarehe 13 mwezi ujao.Bunge la Ujerumani leo linatazamiwa kuamua ikiwa muda wa vikosi hivyo kubakia Afghanistan urefushwe.