PORTOROZ: Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana na Urusi
29 Septemba 2006Mawaziri wa ulinzi wa shirika la NATO wanatarajiwa kukutana na waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Lavrov mjini Portoroz nchini Slovenia, hii leo. Mazungumzo yao yatatuwama juu ya mzozo wa Georgia.
Juma lililopita shirika la NATO liliamua kuzidisha mahusiano na Georgia, lakini taifa hilo lililokuwa la muungano wa zamani wa Soviet, limekuwa na mzozo wa kidiplomasia na Urusi kwa kuwakamata maofisa wanne wa jeshi la Urusi wanaoshukiwa kuwa makachero.
Tangu kukamatwa kwao, jeshi la Georgia limeyazingira makao makuu ya jeshi la Urusi katika mji mkuu Tbilisi. Urusi imemuondoa balozi wake kutoka Georgia na baadhi ya maofisa wake.
Georgia inataka kujiunga na Umoja wa Ulaya na shirika la NATO na imekuwa pia ikifanya juhudi za kuwa na uhusiano wa karibu na Marekani.