1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT PRINCE. Mwanajeshi wa umoja wa mataifa auwawa nchini Haiti.

15 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMk

Mfanyakazi wa umoja wa mataifa ameuwawa nchini Haiti. Mwanajeshi huyo kutoka Ufilipino alipigwa risasi na kuuwawa katika kitongoji kinachomuunga mkono rais Jean-Bertrand Aristide. Wakati huo huo, rais wa serikali ya mpito ya Haiti, Gerard Latortue, amewahakikishia wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanaouzuru nchi hiyo, kwamba uchaguzi utafanyika mwezi Novemba kama ilivyopangwa. Mapema juma hili, tume ya uchaguzi nchini humo ilitangaza uchaguzi huenda ukacheleweshwa kwa sababu ya machafuko yanayoendelea katika taifa hilo.