PORT-AU-PRINCE: Wakati wa kuadhimisha mwaka 200 ...
2 Januari 2004Matangazo
wa uhuru kisiwani Haiti, kulizuka mapigano baina ya wapinzani na wafuasi wa serikali. Askari polisi walitumia hewa ya kutoa machozi mjini Port-au Prince dhidi ya mamia kwa maelfu ya wandamanaji ambao wanamtaka rais Jean-Bertrand Aristide, ajiuzulu. Kiasi wapinzani wawili wa serikali walipigwa risasi. Wakati wa mapigano makubwa baina ya waandamanaji na wafuasi wa Aristide, watu sita wengine walijeruhiwa. Katika mji Gonaives, mlolongo wa magari ulihujumiwa kwa risasi ambao walikuwamo Aristide binafsi na mwenzake wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki. Mjini Gonaives, wananchi wa Haiti walipewa uhuru mwaka 1804 na Ufaransa. Kisiwa hiki cha karibiki kinaagaliwa kama ni maskini kabisa katika eneo la upande wa magharibi.