1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Port-Au-Prince: Mgomo na maandamano yanaendelea kwa siku ya pili ...

10 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkf
mfululizo visiwani Haiti.Lengo ni kumlazimisha ajiuzulu rais Jean-Bertrand Aristide.Msemaji wa serikali mjini Port-au Prince anasema hata hivyo maandamano hayo hayawakilishi maoni ya walio wengi.Shule,benki, vituo vya mafuta ya petroli na baadhi ya mashirika yamefungwa visiwani humo.Hata hivyo watumishi wa idara za serikali na mashirika madogo madogo wanaendelea kwenda makazini.Mvutano umezidi makali visiwani Haiti kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Aristide.Watu wasiopungua wawili wameuwawa wiki hii katika machafuko mjini Prot-au Prince.Washington imewalaumu viongozi wa Haiti wanaotuhumiwa "kuyaachia magengi yanayoungwa mkono na serikali" kuwashambulia waandamanaji wanaodai rais Aristide ajiuzulu.