1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT-AU- PRINCE : Mawaziri wa zamani watoroka gerezani

20 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFcP

Waziri Mkuu wa zamani na waziri wa mambo ya nje wa utawala ulioangushwa wa serikali ya Jean Betrand Aristide ambao walitoroka kutoka gerezani hapo mapema wamekamatwa tena na polisi.

Polisi katika mji mkuu wa Port-au-Prince imesema Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Haiti Yvon Neptune na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Jocelerme Privert walikamatwa masaa machache baada ya kutoroka ambapo polisi iliweza kuwafuatilia wakiwa wanatafuta hifadhi ya kisiasa katika balozi kadhaa.

Wafungwa 350 walitoroka baada ya genge la wanamgambo wenye silaha wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya kulivamia gereza hilo lilioko karibu na Kasri la Rais.