PORT-AU-PRINCE: Aristide akabiliwa na raia
12 Januari 2004Matangazo
Maelfu ya raia wanaopinga serikali ya Rais Jean-Bertrand ARISTIDE wa Haiti wamezidisha maandamano yao kwa kukusanyika kwa wingi hapo jana katika mji mkuu Port-au-Prince na maeneo mengine ya mikoani ili kujaribu kumlazimisha padiri huyo wa zamani kuondoka madarakani. Wakosoaji wake wanamlaumu kwa kuchelewesha uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwaka jana na kumpa nafasi Bwana ARISITIDE kuongoza nchi bila ya kibali cha wananchi. Kinyume na hapo awali, maandamano hayo ya jumapili yamefanyika bila ya madhara makubwa baada ya watu wapatao 46 kuuliwa katika purukushani zilizotangulia kati ya wafuasi wa kiongozi huyo na wapinzani wake miezi kadhaa iliopita.