1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pompeo amemuita Maduro dikteta ambaye ameiharibu Venezuela

Faiz Musa15 Aprili 2019

Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Mike Pombeo yuko katika ziara ya siku nne katika mataifa washirika wa Mareikani katika Amerika ya kusini ambapo ujumbe wake zaidi unalenga mgogoro wa Venezuela.

https://p.dw.com/p/3GnCU
Peru Mike Pompeo und Martin Vizcarra in Lima
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Mejia

Pompeo alimuita Maduro dikteta ambaye amesababisha kuharibika kwa Venezuela na kuwaathiri vibaya raia wake.

Katika kikao na rais wa Paraguay, Mario Abdo Benkitez katika mji mkuu wa Asuncion ambapo walizungumzia swala la uchumi na mgogoro wa kisiasa nchini Venuzuela na uimarishaji wa demokrasia na namna ya kukabiliana na uhalifu nchini humo, Pompeo alimlaumu Maduro kwa kuharibika kwa taifa hilo na kusema Marekani itashirikiana na Paraguay na mataifa mengine kuhakikisha ustawi na demokrasia inarudishwa Venezuela.

Pompeo alimtaka Maduro kubadilisha mbinu zake na kuliachia taifa hilo pamoja na kumtaka kufungua madaraja na mipaka mara moja kama njia ya kuwajali raia wake wanaokumbwa na hali mbaya.

Mike Pompeo in Kolumbien
Pompeo akiamkua familia ya wahamiaji katika hema lao eneo la La Parada Picha: picture-alliance/AP/F. Vergara

"Kuna mpango wa uchaguzi wa haki na uwazi ndani ya Venezuela na mpango wa kurudisha ukuaji wa biashara ili kurudisha hali ya kawaida ya maisha na nafasi za kiuchumi kwa ustawi wa Venezuela. na kabla haya kufanyika ni lazima uongozi mbaya wa Maduro ukomeshwe. Marekani itaendelea kutumia kila njia ya kisiasa na kiuchumi kuwasaidia watu wa Venezuela, kwa kutumia vikwazo vya kiuchumi na kufutilia mbali vibali vya kusafiri" alisema Pompeo.

Kundi la Lima lizidishe shinikizo

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amesema Paraguay kwa kuwa moja wapo ya nchi kumi na mbili zilizounda kundi la Lima la kuhakikisha amani inarudi nchini Venezuela, Marekani inamtambua rais wa nchi hiyo na viongozi wengine wa Lima kuipigania demokrasia kwa kumshinikiza Maduro kuondoka  Madarakani.

Zaidi aliweka bayana kwamba Paraguay ni mshirika wa Marekani katika jitihada za kumtoa Maduro na kumuweka madarakani kiongozi wa upinzani Juan Guido ambaye alijitangaza mwenyewe kuwa rais wa mpito na kuungwa mkono na mataifa mbali mbali.

Venezuela Stromausfall General Black out
Maduka yamefungwa katika eneo la Guacara nchini VenezuelaPicha: picture-alliance/Zumapress/J.C. Hernandez

Zaidi ya raia milioni tatu wa Venezuela wamelikimbia taifa hilo kwa ukosefu wa chakula, dawa na ugumu wa kimaisha.

Katika ziara yake nchini Peru, Mashariki mwa Amerika ya Kusini Pompeo alimshukuru rais wa taifa hilo Martin Vizcarra kwa kuwahifadhi maelfu ya wakimbizi wa Venezuela.

Vile vile kwa njia ya simu alizungumza na waziri wa maswala ya kigeni wa Brazil Ernesto Araujo na kuhakikisha urafiki wa karibu baina ya Marekani  na Brazil na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja kushughulikia mzozo wa Venezuela, athari za mzozo huo kwa mataifa jirani na haja ya kuzikabili nchini zinazomuunga mkono Maduro kama Urusi, Cuba na China.

(AFPE/APE)