1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Ufaransa yakamata tani 1.8 ya kokeini

2 Mei 2024

Polisi wamefanikiwa kunasa tani 1.8 za madawa ya kulevya aina ya kokeini kutoka katika mashua iliyokuwa imetia nanga kwenye bandari ya Marigot huko kisiwani Saint Martin kilicho katika utawala wa Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4fP9T
Gunia na kokeini
Wakala wa dawa za kulevya akiwa amebeba gunia lenye dawa zilizokamatwa, huku mawakala wakijiandaa kuharibu dawa hizo, nje kidogo ya Jiji la Panama.Picha: Arnulfo Franco/AP/picture alliance

Vyanzo vinaeleza kuwa wahusika katika chombo hicho ambacho kinaelezwa kuwa na injini yenye nguvu kubwa, ambayo inatumiwa sana na wasafirishaji wa magendo walitoroka kabla ya kutiwa nguvuni.

Waendesha mashtaka wa umma katika kisiwa hicho cha Ufaransa cha Guadeloupe wametoa ridhaa ya uchunguzi huo kwa mamlaka ya Saint Martin, kaskazini ambayo inatawaliwa na Ufaransa huku kusini mwa kisiwa hicho ni Uholanzi.

Mwaka 2022, mamlaka ya Ufaransa ilinasa tani 27.7 za kokaine, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kwa 2021 ingawa muongo uliopita umeshuhudia ongezeko mara tano zaidi, madawa mengi yakiwasilishwa na usafiri wa majini.