SiasaAsia
Polisi watumia nguvu kuwazuia waandamanaji Nepal
23 Novemba 2023Matangazo
Hatua imetokana na kutaka kuwadhibiti wafuasi wenye kupigania kurudishwa kwa utawala wa kifalme pamoja na hadhi ya zamani ya taifa hilo ya dola lenye kufuata misingi ya Kihindu.Waandamanaji wakipeperusha bendera ya taifa huku wakiimba kwa maneno ya kumuunga mkono mfalme Gyanendra,walikusanyika pembezoni mwa mji mkuu Kathmandu na kujaribu kuelekea katikati ya mji huo. Polisi waliwazuia na kuwacharaza kwa mijeledi pamoja na kufyetuwa gesi za kutowa machozi na kuwafungulia mabomba ya maji. Waandamanaji hao waliosafiri kutoka maeneo mbali mbali ya Nepal, wanadai kufutwa kwa utawala wa Jamhuri na badala yake urudishwe utawala wa Kifalme. Wanaituhumu serikali na vyama vya kisiasa kwa ufisadi na uongozi ulioshindwa.