1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wakabiliana na waandamanaji nchini Malawi

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2019

Polisi walifukuzana na waandamanaji wa upinzani katika mji mkuu wa Malawi Lilongwe hapo jana, hali iliyosababisha jeshi kuingilia kati. Wapinzani wanapinga matokeo ya uchaguzi wa May 21.

https://p.dw.com/p/3NUwQ
Philippinen Soldaten IS
Picha: Getty Images/J.Aznar

Polisi walifukuzana na waandamanaji wa upinzani katika mji mkuu wa Malawi Lilongwe hapo jana, hali iliyosababisha jeshi kuingilia kati. Wapinzani hao wamekuwa wakiandamana mara kwa mara tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa May 21, wakishinikiza kuondoka kwa mkuu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo Jane Ansah. Maandamano hayo yaliyoratibiwa na kongamano la watetezi wa haki za binadamu yalinuia kuwashirikisha watu milioni moja katika miji mitatu muhimu ya Lilongwe, Blantyre na Mzuzu. Mwandishi aliyeko mjini Lilongwe Golden Matonga amekadiria kuwa mamia kwa maelfu waliitikia maandamano hayo. Ingawa hali ilikuwa ya amani katika miji ya Mzuzu na Blantyre, mjini Lilongwe kulizuka hali ya ghasia kati ya waandamanaji na polisi, ambapo gari moja la maafisa wa usalama lilichomwa moto na maduka kadhaa yaliporwa. Vurugu hizo katika nchi ya Malawi ambayo ina historia ya utulivu, zinafuatia kuchaguliwa kwa rais Peter Mutharika kuongoza muhula wa pili, katika uchaguzi ambao wapinzani wake wanasema umekumbwa na mizngwe.