1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Ujerumani hawendi Lebanon

20 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJs

BERLIN:

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani ameondosha kabisa uwezekano wa ujerumani kutuma vikosi vyake vya polisi nchini Lebanon ikiwa ni sehemu ya vikosi zaidi vya kuhifasdhi amani vya UM.Hii ni kwa muujibu wa mazungumzo na gazeti la DIE WELT lililotoka leo.Kulizagaa uvunmi kwamba, ujerumani ingetuma kikosi cha polisi kusimamia eneo la mpakani kati ya Lebanon na Syria.Mchango wa ujerumani asema, Kanzela Merkel ,utakuwa kuvishauri vikosi vya ulinzi vya Lebanon jinsi ya kuendesha kazi hiyo.

Nae waziri wa ndani wa ujerumani Bw.Wolfgang Schauble ameieleza hali ya usalama nchini Ujerumani ni ya kutia wasi wasi ki nyume na kawaida.hii imefuatia kutiwa nguvuni kwa mlebanon mjini Kiel.Bw.Schauble alionya pia kuwa kizazi kipya cha magaidi kinakua nchini humu.Jana, kijana wa kilebanon,mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa mjini Kiel akitiliwa shaka kupachika bomu katika gari-moshi hapo julai 31.