1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi yachunguza bango "maisha ya weupe ni muhimu"

Saleh Mwanamilongo
23 Juni 2020

Wakati wanaharaki mbalimbali wakiendelea kupiga matukio ya ubaguzi wa rangi duniani, polisi wa England wanachunguza tukio la ndege iliyopita angani ikiwa na bendera yenye maneno (White Lives Matter)

https://p.dw.com/p/3eEA9
USA Washington | Demonstration gegen Rassismus
Picha: Imago Images/ZUMA Wire/M. Brochstein

Ndege hiyo ilijitokeza juu ya mandhari ya uwanja wa Etihad muda mfupi baada ya wachezaji na makocha wa timu zote mbili kupiga magoti uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo wao siku ya Jumatatu tarehe (23.06.2020) ikiwa ni ishara ya kuunga mkono harakati za kupinga ubaguzi wa rangi kwa watu weusi. Ndege hiyo iliuzunguka uwanja huo kwa dakika kadhaa.

Kupitia katika mtandao wa Twitter, polisi huko Lancashire wamesema kuwa kutafanyika uchunguzi wa kina. Hata hivyo bango hilo haraka lililaaniwa na Barnley ambayo imeapa kufanya kazi kikamilifu na mamlaka husika ili kubaini wale wote waliofanya tukio hilo ambalo linaonekana la kibaguzi.

Tukio hilo limekuja wakati ambapo ligi ya kandanda ya England na vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo kuunga mkono harakati za watu weusi za kupinga ubaguzi wa rangi wanaofanyiwa kufuatia kuuwawa na polisi kwaGeorge Floyd huko Minnepolis mwezi uliopita.

Wakati msimu wa ligi kuu ya soka ya England ukirejea tena wiki iliyopita huku kukiwa na mlipuko wa virusi vya Corona harakati za kupinga ubaguzi wa rangi na kukutetea masilahi ya watu weusi, zimebadilisha majina ya wachezaji huku wakiandika ujumbe nyuma ya jezi zao kuunga mkono harakati za watu weusi wanaokabiliwa na vitendo vya kibaguzi.

Wachezaji, makocha pamoja na maafisa wa mechi za ligi hiyo wamekuwa wakipiga magoti kwa takribani sekunde 10 kabla ya kuanza kwa mchezo katika michezo 12 ya kwanza itakayochezwa mara baada kurejeshwa tena masuala ya michezo baada ya kusimamishwa kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona.

Chanzo: AP