1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Tanzania yanyima Upinzani ruhusa

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cklz

DAR-ES-SALAAM:

Polisi nchini Tanzania,jirani ya Kenya,imepiga marufuku maandamano yaliopangwa kufanywa hii leo na vyama 4 vya upinzani ili

Kuonesha umoja na mshikamano na mtetezi wa wadhifa wa urais nchini Kenya Raila Odinga.

Akitoa kielezo kwanini upinzani nchini Tanzania umenyimwa ruhusa ya kuandamana, afisa mkuu wa polisi Alfred Tibaigana alisema,

„Hali isio ya usalama nchini Kenya, imezusha pia wasi wasi wa usalama nchini Tanzania. Kufanya maandamano kuungamkono upande mmoja wa mgogoro uliozuka kutachafua zaidi hali ya mambo.“

Mkuu huyo wa polisi alisema vyama 4 vikuu vya Upinzani nchini Tanzania-Civic United Front (CUF),Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) NCCR-Mageuzi na Tanzania Labour Party (TPL) vilitoa taarifa kwa polisi kuiarifu azma yao ya kuandamana hii leo mjini Dar-es-salaam.

Tibaigana alisema kwamba vyama hivyo 4 vya upinzani vimekataa hata hivyo, kuyavunja maandamano yao.Akasema polisi imewataka wakaazi wa jiji la Dar-es-salaam kuyasusia maandamano hayo .