1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi nchini Kenya wawasaka wafuasi wa Al Shabab

18 Januari 2010

Wafuasi wa kundi la Al Shabab wasakwa na polisi katika kitongoji cha Eastleigh,Nairobi.

https://p.dw.com/p/LYnk
Kitongoji cha Eastleigh kilichovamiwa na polisiPicha: picture-alliance/dpa

Maafisa wa polisi nchini Kenya usiku wa kuamkia leo wameuvamia mtaa wa Sherif katika kitongoji cha Eastleigh kuwasaka wafuasi wa kundi la Al Shabab walioshiriki kwenye maandamano ya Ijumaa wiki iliyopita kushinikiza kuachiwa huru kwa shehe wa kutoka Jamaica, Sheikh Abdullah al Faisal, anayezuiliwa nchini humo.

Josephat Charo amezungumza na Bwana Omar Hassan, mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya kuhusu uvamizi huo.

Mtayarishi: Josephat Charo

Mhariri: Othman Miraji