Sheria na HakiMarekani
Polisi aliyemuua George Floyd ajeruhiwa jela
25 Novemba 2023Matangazo
Afisa wa polisi aliyemuuwa Mmarekani mweusi George Floyd ambaye kifo chake kilichochea vuguvugu kubwa la kupinga ubaguzi wa rangi amejeruhiwa vibaya katika jela ya shirikisho kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Gazeti la Marekani la NewYork Times limesema kuwa Derek Chauvin alichomwa kisu jana katika jela la Tucson huko Arizona lakini amenusurika baada ya kuwahishwa hopistali kwa matibabu.
Kifo cha George Floyd kilichotokea Mei 25 mwaka 2020, kilisababisha maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ghasia za polisi kote nchini Marekani na sehemu mbalimbali duniani. Polisi aliyemuua alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama za jimbo la Minnesota na kuhukumiwa kifungo cha miaka 22 jela.