1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Polisi 200 zaidi wa Kenya waelekea Haiti

16 Julai 2024

Maafisa wengine 200 wa polisi wa Kenya waliondoka Jumatatu usiku kuelekea Haiti, chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unaolenga kumaliza ghasia za magenge ya wahalifu katika taifa hilo la Caribbean.

https://p.dw.com/p/4iM7x
Kikosi cha polisi Kenya kinachoenda Haiti
Kenya inaongoza kikosi cha kimataifa cha polisi kinachohudumu nchini Haiti.Picha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Maafisa wengine 200 wa polisi wa Kenya waliondoka Jumatatu usiku kuelekea Haiti, chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unaolenga kumaliza ghasia za magenge ya wahalifu katika taifa hilo la Caribbean.

Soma pia: Kikosi cha kulinda amani Haiti chaahidi kuleta utulivu

Taarifa hii imetolea na maafisa wakuu wa polisi wa Kenya waliosema kuwa zoezi hilo litaendelea hadi kufikia idadi ya polisi 1,000. Kundi la kwanza la maafisa 400 waliwasili Haiti mwezi Juni.

Soma pia: Kikosi cha Kenya chajitolea dhidi ya magenge Haiti

Kwa miaka mingi Haiti imekuwa ikikabiliwa na uhalifu wa magenge wa watu wenye silaha ambayo kwa sasa yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince na pia barabara kuu katika nchi hiyo maskini ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa pia na misukosuko ya kisiasa.