Poland yafanya uchaguzi wa duru ya pili
4 Julai 2010Warsaw.
Wananchi nchini Poland wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa rais uliosababishwa na kifo cha rais wa nchi hiyo Lech Kaczynski kutokana na ajali ya ndege. Inaonekana kuwa uchaguzi huo utakuwa na ushindani mkubwa kati ya mdogo wake marehemu rais Kaczynski, Jaroslaw, ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani, pamoja na rais wa muda mliberali Bronislaw Komorowski, kutoka chama tawala cha Civic Platform. Kura ya mwisho ya maoni inaonyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na ushindani mkubwa. Katika duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Juni 20 , Komorowski alipata asilimia 41.5 ya kura , ikilinganishwa na asilimia 36.5 alizopata Kaczynski. Uchaguzi wa leo unaonekana kuwa mtihani muhimu kabla ya uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika mwakani 2011.