1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kutia saini mkataba wa Lisbon

Sekione Kitojo10 Oktoba 2009

Rais wa Poland Lech Kaczynski anatarajiwa leo hii kutia saini mkataba wa umoja wa Ulaya unaojulikana kama mkataba wa Lisbon.

https://p.dw.com/p/K3T0
Rais wa Poland Lech Kaczynski ambaye hatimaye ataidhinisha mkataba wa Lisbon leo.Picha: picture-alliance/dpa

Rais wa Poland Lech Kaczynski hii leo atatia saini mkataba wa Umoja wa Ulaya uliyofanyiwa marekebisho na kujulikana kama Mkataba wa Lisbon. Sherehe hiyo katika ofisi yake mjini Warsaw inatazamiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Bunge la Ulaya Jerzy Buzek, Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso na Waziri Mkuu wa Sweden Fredrik Reinfeldt.

Mkataba wa Lisbon ulikwisha idhinishwa na mabunge yote mawili ya Poland tangu mwezi wa Aprili. Lakini Kaczynski aliamua kungojea matokeo ya duru ya pili ya kura ya maoni nchini Ireland kabla ya kutia saini mkataba huo. Poland na Jamhuri ya Czeki ni nchi mbili za mwisho katika Umoja wa Ulaya zinazosubiriwa kutia saini mkataba huo.

Sasa Rais wa Jamhuri ya Czeki Vaclav Klaus anapaswa kutia saini yake ili Mkataba huo wa Lisbon uweze kutumika.