Poland kurejesha nyumbani wanajeshi wake kutoka Irak
23 Novemba 2007Matangazo
Poland inatazamia kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake wote 900 kutoka Irak ifikapo mwisho wa mwaka 2008.Waziri Mkuu mpya wa Poland Donald Tusk, alitamaka hayo leo hii,alipohotubia Bunge la Poland kwa mara ya kwanza tangu kushika wadhifa wake.Akaongezea kuwa wanajeshi 1,200 waliopo Afghanistan watabakia huko.