Poland inapanga kuwarejesha nyumbani wanajesgi wake toka Irak
12 Aprili 2005Matangazo
Warschau:
Poland inapanga kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake toka Irak hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu.Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Poland JERZY SZMAJDZINSKI,muda wa shghuli za tume ya umoja wa mataifa nchini Irak utakapomalizika,litakamilika pia jukumu la wanajeshi 1700 wa Poland nchini humo.Wanajeshi wa Poland wanaongoza vikosi vya wanajeshi 4000 wa kimataifa kusini mwa Baghdad.Poland imepunguza zaidi ya nusu ya wanajeshi wake mara tuu baada ya chaguzi za kwanza huru kumalizika nchini Irak.