1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Platini asema idadi ya timu za kombe la dunia iongezwe

28 Oktoba 2013

Kiongozi wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA Michel Platini anataka dimba la Kombe la Dunia lipanuliwe hadi timu 40 kuanzia mwaka wa 2018 ili kuzipa nafasi nchi nyingi za Afrika na Asia kushiriki

https://p.dw.com/p/1A7R9
Picha: picture-alliance/dpa

Bara la ya Ulaya kwa sasa hutoa timu 13 kati ya 32 zinazoshiriki katika tamasha hilo, ikilinganishwa na timu tano kutoka Afrika na nne au tano kutoka bara la Asia, kulingana na washindi wa mchuano wa mchujo dhidi ya timu moja ya Amerika ya Kusini. Platini amesema badala ya kupunguza timu ya Ulaya, ni vyema kuongeza timu nane kwa zile 32 zinazoshiriki Kombe la Dunia

Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA Sepp Blatter aliandika wiki iliyopita kuwa mabara ya Afrika na Asia yanastahili uwakilishi zaidi katika tamasha hilo la soka kwa sababu yana mashirikisho mengi wanachama kuliko Ulaya na Amerika ya Kusini. Platini anayeonekana kuchukua nafasi ya Sepp Blatter kama mkuu wa FIFA, anasema hesabu zake zinaonyesha kuwa kwa kuongeza timu nane kutamaanisha kuwa dimba hilo liongezwe kwa siku tatu pekee.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu