Plastiki nchini Kenya: Kutoka biwi la takataka hadi tumboni
Sheria inayopiga marufuku mifuko ya plastiki nchini Kenya imeanza kutekelezwa. Katika eneo kubwa la kutupa taka nchini humo, unaweza kuona jinsi takataka za plastiki zinaweza kuingia katika vyakula vinavyouzwa.
Faida kutokana na takataka
Wanaokusanya takataka wakipekuapekua na kutafuta takataka ambazo zinaweza kutumiwa tena katika eneo kubwa la kutupa takataka la Dandora katika mji mkuu wa Kenya- Nairobi.
Takataka kupita upeo wa macho
Dandora ndiyo sehemu yenye rundo kubwa la takataka mjini Nairobi. Watu wengi hupata riziki yao kwa kuokota vile vitu ambavyo wengine wametupa hapa.
Mzigo mzito
Waokotao takataka wanalipwa kulingana na uzani wa takataka walizokusanya. Kuna bei rasmi kwa kila kilo ya aina ya takataka kama glasi, plastiki na vyuma. Katika siku nzuri, anayeokota takataka anaweza kupata takriban euro 3 ambazo ni kama shilingi mia tatu za Kenya.
Karamu kwa ndege
Takataka nyingi huwa ni za plastiki, ikiwemo mifuko mingi isiyohesabika ya sandarusi inayotumiwa kubeba bidhaa kutoka madukani. Wanyama na ndege pia hujifaidi kutokana na takataka hizo zinazopatikana Dandora: ndege hawa aina ya Marabou storks hupata vyakula vingi hapa.
Mlo wetu unakula takataka
Ng'ombe hawa pia wanakula takataka ambazo ni vyakula asilia kwao, ila takataka hizo zinapatikana miongoni mwa takataka za plastiki.
Kutoka katika rundo la takataka hadi machinjioni
Baadhi ya ng'ombe ambao wamekuwa wakila katika rundo la takataka la Dandora, baadaye huishia machinjoni
Marejeo ya plastiki
Mifuko ya plastiki hukutwa katika matumbo ya ng'ombe hao ambao huchinjwa na nyama kuuziwa watu kama chakula. Inatarajiwa kuwa marufuku kwa mifuko ya plastiki itapunguza hatari za kiafya kama hii na pia athari za kimazingira.